Waandishi wa habari mwanza wapigwa msasa

WAANDISHI wa habari jijini hapa wametakiwa kujikita kwenye uandishi wa habari za madini ili kuimarisha na kutetea demokrasia , uwajibikaji na utawara bora katika masuala ya na sekta ya madini na uwekezaji.

Katika kuhakikisha hilo linafanyika kwa ufanisi Shirika la Action for Democracy and Local Government (ADLG) limetoa mafunzo kwa wanahabari ili kutoa elimu kwa na kuwajengea uwezo watu wanaoishi karibu na uwekezaji wa migodi hususani katika wilaya za Kahama, Kishapu na mkoani Geita.

Mkurugenzi wa Shirika hilo Jimmy Luhende alisema kuwa licha ya kanda ya ziwa kuwa na maeneo mengi ya migodi lakini wananchi wake husasani wanaozungukwa na migodi hiyo wamekuwa masikini kwa kutokujua sera na sheria za madini ikiwa na ukisefu wa waandishi mahiri wa habari hizo.

“Nataka niwajengee uwezo waandishi wa habari wa kanda hii ili waweze kuwa na uwezo wa kuandika masuala ya madini ikiwa na kuwaandaa kupata tuzo za mwandishi bora wa makala za sekta hii muhimu hapa nchini zitolewazo na Baraza la Habari (MCT)”, alisema Luende.

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Fredreck Katulanda alisema kuwa ni muda muafaka sasa wanahabari kutumia fursa hii ili kujua namna ys kuripoti kazi za migodini kuokana na baadhi ya migodi hiyo kuwa na changamoto nyingi.

“ Waandishi wenzangu naamini mafunzo  haya yanayotolewa na ADLG yatawajenga kitaaluma kwani baadhi ya waandishi hawajui namna ya uandikaji wa habari hizi”,  alisema Katulanda.

Akiongea baada ya mafunzo hayo mmoja wa waandishi wa habari George Binagi alisema anashukuru kutolewa kwa mafunzo haya kwani yamemjenga kitaaluma na namna ya kufanya kazi kwenye sekta ya madini.

Mwisho.

 Imeandikwa na Oscar Mihayo

Leave a Reply