WANANCHI WAMUOMBA MBUNGE KANYASU KUINGILIA KATI MADAI YAO YA FIDIA DHIDI YA MGODI WA GGM.
Wakazi wa mtaa wa Nyamalembo mjini Geita wamemuomba Mbunge wa Geita mjini Bw Constantine Kanyasu kuingilia kati tatizo lao la muda mrefu la kutolipwa fidia na mgodi wa dhahabu wa GGM na kunyimwa nafasi ya kufanya shughuli za kilimo kwa madai kuwa wako kwenye eneo la mgodi hali inayoendelea kuwarudisha nyumba kimaendeleo.
Wakizungumza kwenye mkutano wa maendeleo katika mtaa huo mbele ya mbunge wananchi hao Bw Charles Methew na Juma Bakari wamesema wameendelea kupokea ahadi za viongozi uong kutoka kwa viongozi ambao wamekwisha kuja kwenye maeneo yao na kujionea namna ambavyo mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM)ulivyo haribu makazi yao kutokana na shughuli ambazo wanazifanya za ulipuaji wa miamba pia wameelezwa kusikitishwa na namna ambavyo wamekuwa wakizuiliwa kulima kwenye maeneo hayo na pindi wanapokamatwa wamekuwa wakipigwa na askari wa mgodi hali ambayo wamemwambia mbunge kua imekuwa ikiwaumiza sanaa.
Diwani wa Kata ya Mtakuja Bw Constatine Molandi alisema mwambia Mbunge kuwa licha ya neema ya uwepo wa mgodi wananchi ambao wanauzunguka mgodi huo wanamatatizo makubwa sanaa na kwamba kilio chao kilishawai kufikishwa kwa Rais Magufuli lakini bado wameendelea kuonewa na kunyimwa fidia na watu wa mgodi huo ali ambayo imesababisha kujiona kama vile wao sio watanzania.
Kufuatia malalamiko hayo Mbunge wa Geita Mjini Bw Constatine Kanyasu amewataka wananchi wa maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za mgodi wa dhahabu wa GGM kuwa wavumilivu kwani madai yao ya kulipwa fidia yamefikishwa kwenye wizara husika na kwamba madai hayo yatafika na kwa mheshimiwa Rais John Magufuli.
IMEANDALIA NA MADUKA ONLINE MEDIA