Waandishi wa habari wapigwa msasa

WAANDISHI wa habari jijini hapa wametakiwa kujikita kwenye uandishi wa habari za madini ili kujinyakulia tuzo za umahiri zinazotolewa kila mwaka na baraza la habari nchini (MCT). Hatua hiyo imekuja baada ya kutokuwa na mwandishi mahiri  kanda ya ziwa aliepata tuzo ya masuala ya madini huku kanda hiyo ikiongoza kwa  migodi hapa nchini.

Aidha Mafunzo hayo yametolewa na Shirika la Action for Democracy and Local Government (ADLG)  ikiwa ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kubobea kwenye masuala hayo na kuwa washindi wa tuzo za umahiri kwenye sekta ya madini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Shirika hilo Jimmy Luhende  amesema mafunzo hayo yatawasaidia waandishi  katika kuandika habari pamoja na kupata ushindi wa tuzo.

“Mafunzo haya yanayotolewa na ADLG yatawajenga kitaaluma baadhi ya waandishi hawajui namna ya uandikaji wa habari hizi na huko migodini kuna chnagamoto nyingi  kwa hiyo ni fursa ya pekeekwa waandishi waliopata mafunzo kuitumia vizuri”amesema Katulanda.

Akiongea baada ya mafunzo hayo mmoja wa waandishi wa habari Shabani Juma amesema mafunzo hayo yatawajenga kitaaluma na namna ya kufanya kazi kwenye sekta ya madini.

Mwisho.

Imeandikwa na Anna Fredy